Nenda kwa yaliyomo

Doug Burgum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Doug Burgum (Alizaliwa 1 Agosti, 1956) ni mfanyabiashara na mwanasiasa nchini Marekani ambaye amehudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani tangu mwaka 2025 chini ya Rais Donald Trump.[1] Alihudumu kama Gavana wa North Dakota kuanzia mwaka 2016 hadi 2024.[2] Kabla ya siasa, alikuwa mfanyabiashara katika tasnia ya programu za kompyuta; aliuza kampuni yake, ya Great Plains Software, kwa Microsoft mwaka 2001 kwa dola bilioni 1.1.[3] Mnamo Novemba 2024, Rais Trump alimteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, na alithibitishwa na Seneti ya Marekani kwa kura 79 dhidi ya 18 mnamo Januari 2025.[4]

  1. "President-elect Trump nominates Burgum to serve as Interior Secretary, chair new National Energy Council". North Dakota State Government.
  2. "Doug Burgum elected Governor". WDAY. November 10, 2016.
  3. "Microsoft Completes Acquisition of Great Plains" (Press release). Microsoft Corp. April 5, 2001.
  4. Budryk, Zack (January 30, 2025). "Senate confirms Burgum as Interior secretary". The Hill.